Advertisement

COVID-19 Translation - Kiswahili

(KBTX)
Published: Apr. 13, 2020 at 10:59 AM CDT
Email this link
Share on Pinterest
Share on LinkedIn

Habari na karibuni kwenye mkondo huu wa moja kwa moja kupitia Facebook live kutoka

Multi-Cultural Center. Mimi ni Sadik Muhammad, ninafanya kazi kama mkalimani wa

Multi-Cultural Center.

Mkondo huu wa livestream ni sehemu ya vipindi tunavyofanya ili kutuma habari muhimu

kuhusu COVID19 kwa jamii tofauti zisizofahamu kiingereza hapa jijini Sioux Falls.

Ugonjwa wa Coronavirus 2019 (COVID-19) ni ugonjwa wa kupumua ambao unaweza kuenea

kutoka kwa mtu hadi mtu.

Wagonjwa walio na COVID-19 wamekuwa na ugonjwa wa kupumua na dalili zake ni:

• homa ya digrii 100 au zaidi

• kikohozi

• upungufu wa pumzi

Katika hali mbaya, wagonjwa wengine huwa na nimonia katika mapafu yote mawili, kushindwa

kwa viungo vingi na katika visa vingine vifo.

Virusi huenea kati ya watu ambao huwasiliana wakiwa karibu (yaani chini ya fiti 6) kupitia

matone ambayo hutolewa wakati mtu aliyeambukizwa anakohoa au kupiga chafya.

Inawezekana pia kwa mtu hupata COVID-19 kwa kugusa uso au kitu ambacho kina virusi juu

yake na baadae kugusa pua, macho, au midomo yao.

Hakuna chanjo dhidi ya COVID-19 na hakuna tiba maalum ya kukinga-virusi. Watu walio na

COVID-19 wanaweza kutafuta huduma ya matibabu ili kusaidia kupunguza dalili.

Watu wazee na watu walio na hali ya msingi ya kiafya wanaweza kuwa katika hatari kubwa

kutoka kwa COVID-19.

Ili kujikinga na kuzuia kuenea kwa virusi hivi:

• Jiepushe na mawasiliano ya karibu na watu ambao ni wagonjwa.

• Jiepushe na mikusanyiko mikubwa ya kijamii ya watu 10 au zaidi na epuka mawasiliano ya

kimwili (kwa mfano kukumbatiana, kushikana mikono na kadhalika), ukibaki angalau fiti 6 mbali

na watu wengine. Hii ndio sababu ya shule na biashara zimelazimika kufunga au kupunguza

huduma zao.

•Jiepushe na safari zote ambazo sio muhimu, kwa mfano, safari za kijamii au safari za ununuzi

madukani. Kwenda kwenye duka la mboga kutumika. Usafiri mwingine muhimu ni sawa lakini

kama sheria ya jumla unapaswa kukaa nyumbani.

• Jiepushe kugusa macho, pua na mdomo wako kwa mikono michafu.

• Osha mikono yako mara nyingi kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20. Tumia sanitizer

inayotokana na alcohol ya kiwango cha asili mia 60 ikiwa sabuni na maji hazipatikani.

• Funika kikohozi chako au kupiga chafya na tishu, kisha tupa tishu hizo kwenye takataka.

• Safisha sehemu unazogusa kwa mikono mara kwa mara.

Kama wewe au mtu wa familia yako ni mgonjwa, hasa kama wewe au wao wanahisi dalili za

COVID-19 kama vile kikohozi, homa au upungufu wa kupumua:

● Kaa nyumbani, punguza kukaa karibu na wengine (kukaa katika chumba kimoja, mbali na

watu wengine ndani ya nyumba yako, tumia choo tofauti ikiwezekana, jiepushe kutumia

vitu vya kibinafsi pamoja)

● osha mikono yako mara kwa mara

● pumzika na kunywa maji kwa wingi

● safisha sehemu za matumizi mara kwa mara

● piga simu kwa daktari wako kabla ya kwenda kliniki.

Ikiwa umesafiri hivi karibuni kutoka nchi au eneo lenye COVID-19:

● piga simu kwa daktari wako na umwaambie kuhusu safari yako ya hivi karibuni.

Watakushauri juu ya nini cha kufanya.

● Unaweza kulazimika kujitenga nyumbani na kuzuia harakati zako kwa mda wa wiki 2.

Ikiwa unahitaji msaada hatua kuu ya mawasiliano hapa mjini Sioux Falls kwa habari juu ya

msaada wa dharura ni Kituo cha Helpline Center. Ikiwa unahitaji msaada lakini haujui ni wapi

utapata msaada, piga simu 2-1-1 kisha bonyeza "2" au tembelea www.helplinecenter.org/ .

Unaweza pia kupigia simu Multi-Cultural Center kwa 605-367-7401.

Ikiwa unahitaji chakula au usambazaji wa mahitaji ya msingi:

● Wilaya ya Sioux Falls School itaendelea kutoa chakula BURE chakula cha asubuhi na cha

mchana kwa muda wa shule zitakapokuwa zimefungwa, kuanzia saa 11:30 za asubuhi -

hadi saa 12:30 za mchana kwa mtoto yeyote mwenye umri wa mwaka 1 hadi 18. Milo hii

itakuwa chakula cha mchana cha kuchukua nyumbani kwenye mifuko ambayo inaweza

kuchukuliwa na kupelekwa nyumbani kula.

o Sehemu za Chakula cha mchana ni: Laura B. Anderson, Hawthorne, Hayward,

Anne Sullivan, Terry Redlin, na Lowell Elementary Schools.

o Maelezo kamili yanapatikana katika smore.com/ah6sh

● Feeding South Dakota wanayo program ya chakula cha kupiga simu : chakula kitakuwa

katika visanduku na mifuko na vitasambazwa kwa mtindo wa drive-thru. Angalia tovuti

ya www.feedingsouthdakota.org kwa ratiba kamili.

● Chakula cha Sioux Empire cha watoto watapanga namna ya kukuletea chakula

nyumbani kwako. Tembelea tovuti hii completemediainc.com/food-for-se-kids kwa

maelezo zaidi.

● Corona Help SF itatoa mahitaji ya msingi kwa nyumba yako na itakuwa na chakula

kinachopatikana cha kuchukua. Tembelea tovuti hii ya

www.coronahelpsf.com/i-need-help kwa maelezo zaidi.

Kwa maswala ya makazi:

● Meya wa Sioux Falls, mheshimiwa Paul TenHaken, ametuma barua kwa watoa huduma

wote wa makazi ndani ya Sioux Falls kuwasihi washirikiane na wapangaji wao kwa

kuchelewesha kumfukuza mtu yoyote kutokana na changamoto za kifedha

zilizosababishwa na COVID-19. Ikiwa unahitaji msaada juu ya maswala ya makazi

tafadhali wapigie simu Multi-Cultural Center kwa nambari hii 605-367-7401.

Ikiwa umefutwa kazi au masaa yako ya kazi yamepungua kwa sababu ya COVID-19:

● Meya ameanzisha msaada unaoitwa One Sioux Falls Fund ambao unaweza kuomba

msaada wa kifedha. Piga simu kituo cha msaada kwa namba 2-1-1 kisha bonyeza "2" au

utembelea tovuti hii www.helplinecenter.org/

● Kuomba msaada wa ukosefu wa ajira, piga simu kwa Idara ya Kazi ya jimbo la SD kwa

namba hii 605-773-3101 au tembelea tovuti ya dlr.sd.gov .

● Jumuiya ya Katoliki inayo programu ya kutoa msaada wa kifedha. Wasiliana na mkuu wa

kanisa lako au mchungaji kwa maelezo zaidi.

● Ikiwa ulijaza ushuru au taksi ritani ya mwaka 2018 au 2019, serikali ya Amerika itakuwa

ikituma malipo ya wakati mmoja kwenye benki akaunti yako ya hivi karibuni uliojazia

taksi ritani. Kwa yeyote anayepata mshahara wa hadi $75,000 pesa zake zitakuwa:

o $1200 kwa mtu

o $2400 kwa wanandoa

o Dola ya ziada ya 500 kwa kila mtoto chini ya miaka 16 aliyejumuishwa kwenye

taksi yako.

Huo ndio mwisho wa live stream yetu leo. Asante Dakota News kwa kutusaidia kwa hili.

Ikiwa unahitaji msaada juu chochote nilichozungumza leo tafadhali wasiliana na Multi-Cultural

Center kwa nambari 605-367-7401.

Asante nyote kwa kutazama, tunatumai kuwa habari ambayo tumetoa ni muhimu - usisahau

kuosha mikono yako, kujiepusha mbali na watu na zaidi ya yote, ubaki salama!

Latest News

Latest News